TUYAJALI MAZINGIRA

 1. Jukwaa twaingia, tayari kuwaelimisha,
  Jukumu twajipatia, mradi kuwajulisha
  Tusije tukajutia, lengo letu kuwahamasisha
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

 2. ‘Chafuzi wa mazingira, ni mbaya kutazama,
  machoni inatukera, katu si jambo jema,
  Tena yake maadhara, siyo mazuri daima,
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

 3. Kutupa ovyo taka, inachangia uchafuzi,
  Mijiniau vichaka, ni mbaya waziwazi,
  Tumeivuka mipaka, watoto kwa wazazi,
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

 4. Uchafuzi huu jameni, unaleta vifo vingi,
  Aina za saratani, zatuua kwa wingi,
  Mwisho tabaki nani, mapema ‘sipojigangi?
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

 5. Recycle nd’o jibu, shida kutatuana,
  Kubwa hasa sababu, zipate kutumika tena,
  Tukifanya kiadabu, ‘tapata kazi vijana,
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

 

 1. Kusafisha huu uchafu, yaweza kutusaidia
  twaweza pata sarafu, hata za kigeni pia,
  uchumi wetu hafifu, kifedha tukaimarishia,
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

 2. Kwa waziri Tobiko, ni we’ twategemea,
  Jukumu ni lako, kazini usije legea,
  Nasi tuko kando yako, nguvu zetu ‘ongezea,
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

 3. Hongera kwenu NEMA, kaziyo watambua,
  Nchi ‘metendea mema, kweli mumeamua,
  Wenyewe mumejituma, plastiki ‘timua,
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

 4. Ni letu sote jukumu, kutupa vyema taka,
  Isije ikawa sumu, tukawa wake mateka,
  Mikakati ya kudumu, ‘nahijati kuiweka,
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote

 5. Shairi ‘mehitimisha, jukwaa tunaondoka,
  Ujumbe ‘meifikisha, dua letu ‘mesikika,
  Tujitolee kusuluhisha, nchi ipate ‘nufaika,
  Tuyajali mazingira, ni jukumu letu sote.

Owino Ooko

 

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s