PONGEZI MWALIMU

 1. Hizi zangu shukrani, ‘toka moyonimwangu,
  Kweli nakuthamani, mdogo nikiwa tangu,
  Ninaweza kupa nini, ewe baraka wa Mungu?
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia

 2. Busara umenijaza, akilini ‘siyafute,
  ‘Menitoa kwa giza, nasema wajue wote,
  Ujinga umefukuza, mabaya yasinipate,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia.

 3. Adabu umenitia, amani nakaa na jamii,
  Sifa nakumiminia, wala katu sikutanii,
  ‘Taishi kusimulia, ‘livyonifunza bidii,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia

 4. Mshahara ninapata, zotezo zako juhudi,
  Kama nyota nitameta, ‘tajitahidi zaidi,
  Nyayo zako ‘tafuata, kwao niwe shahidi,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia.

 5. Chuo au chekechea, kote ‘menielimisha,
  Dunia naelezea, mahali ‘menifikisha,
  Kistadi umenilea, mawazo ‘menisafisha,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia.

 6. Jua ‘mestahimili, ili nipate elimu,
  Upepo na mvua kali, hazikukutoa hamu,
  Daima ulinijali, kwa mapenzi yal’odumu,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia.

 7. Mawaidha ‘linijaza, njia nisije potea,
  Darasa nilipocheza, ukali ‘linitolea,
  Daima uliniagiza, masomo kutozembea,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia

 8. Ulikuwa ‘fano bora, kwa’lo nakushukuru,
  ‘Litaka nisiwe ‘kora, taabu ‘kaninusuru,
  Kwangu yako seera, kwa jamii niwe nuru,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia.

 9. Ukapateheri njema, na baraka zake Mungu,
  Zidi ‘watendea mema, watoto na ‘jukuu wangu,
  Utajazwa neema, zile tokazo mbingu,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia.

 10. Imeisha yangu zamu, jukwaa ninaondoka,
  Kilichoko cha muhimu, tuwapendeni hakika,
  Tusiwape pesa adimu, wasije kuteseka,
  Pongezi ‘we mwalimu, daima nakusifia.

Owino Ooko

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s