BIMA YETU SUPER COVER

 1. Bima afya nchini, debe tunaipigia,
  Mijini hadi ‘shinani, wote twajivunia,
  Hata wal’o masikini, tiba inawafikia,
  Bima yetu supacover, baraka kwawakenya.
 2. Wanazo tele huduma, kutosha kila mmoja,
  Usije jishika tama, hata ndwele zikija,
  Bora uanze mapema, maradhi hayawi hoja,
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.
 3. Wanayo ndoto kamili, kuwa bora yao nia,
  Jukumu lao asili, sote tunashabikia,
  Wala bado hawajafeli, kazini ‘wajibikia,
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.
 4. Ukitaka ‘pasuaji, fahamu utalipiwa,
  Mwenyewe utajaji, , jinsi utahudumiwa,
  Tena hautahitaji, muchango wa kutibiwa,
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.
 5. Watu wote familia, supacover kawacover,
  Hakuna tena kulia, hata ukipata fiva,
  Kote ‘takuhudumia,kazi tamu kama pizza.
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.
 6. Wamama waja’ wazito, rahisi kujifungua,
  Kitambo ‘likuwa ndoto, gharama wametimua,
  Ndiposa huu wito, siri tumegundua,
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.
 7. Wale watakaofiwa, hawana cha kuwahofu,
  Mazishi utalipiwa, heshima ‘tapata mufu
  Wal’obaki kufidiwa, wasije kuwa hafifu,
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.
 8. Mia tano kwa mwezi, upate kinga kamili,
  Usidhani ni upuzi, NHIFu wanajali,
  Wala usitoe chozi, eti we’ hauna mali,
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.
 9. Changamoto wako nazo, baadhi tumesikiya,
  Ufisadi nd’o chanzo, wengine wanaibiya,
  Vyote hivi ‘kwazo, bado tunawasifiya,
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.
 10. Tunawarayi ‘nzetu, huu ndio wakati,
  Tuyajali maisha’tu, tuwekeni mikakati,
  Tuwalete wenzetu, wote ndani tufiti,
  Bima yetu supacover, baraka kwa wakenya.

Owino Ooko

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s